Charles Venny

Informações:

Sinopsis

Hi, welcome to the Charles venny podcast. Get to hear what you will love.

Episodios

 • Utapoteza Account zako za Google

  21/05/2023 Duración: 20min

  “Use it or Lose it” Google wanakwambia “Tumia au Ipoteze”. Wanaongelea zile accounts ambazo zimekaa muda mrefu bila kutumika. Hizi account zote zitafutwa bila kujali kama mmiliki yuko hai au tayari amefariki.

 • Google Chrome CAPTCHA kuondolewa katika Version Zijazo

  08/05/2023 Duración: 13min

  CAPTCHA imekuwa ni kitu inakera sana hivi karibuni pale inapokuja mara kwa mara. Kila muda inakutaka kuthibitisha kama wewe ni binadamu. Ni kama vile bots zimeanza kuichukua dunia, lakini haiko hivyo.

 • Google kubadili icon ya HTTPS kwa sababu imepoteza uhalisia wake

  04/05/2023 Duración: 11min

  Mwanzoni mwa miaka ya 2010s kufuli iliyofungwa ilianza kutumika kuonyesha kwamba website ziko salama. Miaka ya sasa hivi alama hii imeonekana kupoteza thamani yake kwa kuwa hata website zenye malicious code zinaonekana kutumia alama hii. Hivyo google wameamua kuja na utatuzi mpya wa tatizo hili.

 • Namna mitandao ya kijamii inasikiliza kila unachoongea

  18/04/2023 Duración: 26min

  Sio mara moja watu mtandaoni wamelalamika kwamba mitandao ya kijamii inasikiliza mazungumzo yao. Hiyo ni kwa sababu huwa wakizungumza kuhusu jambo wanaanza kuona matangazo kuhusu hicho kitu. Kuna namna ambayo mitandao ya kijamii inasikiliza mazungumzo yako, lakini sivyo hivyo unavyofikiria .

 • Kifo Cha Google Launcher

  08/04/2023 Duración: 10min

  Miaka yote google wamekuwa mstari wa mbele katika kutoka bidhaa/software ambazo zinapendelewa na watu. Imekuwa ni kampuni ambayo ikiona software haiko vizuri wanaiondoa sokoni na kuleta nyingine. Sasa hivi ni zamu ya kuiondoa kabisa Google Launcher.

 • Facial Recognition: Inakuja na Maajabu Gani?

  19/01/2023 Duración: 22min

  Kwa miaka mingi tumeona Facial Recognition ikitumika katika movies na tukatamani sana kuona namna inavyofanya kazi katika uhalisia. Wakati tukitamani sana kuona God's eye ya Fast and Furious kuwa ya kweli tayari kuna tech za facial recognition zinatumika duniani. Furaha ipo kwa mamlaka zinazohusika na kukaa na data zinakusanywa hapa, lakini kwa wananchi ni shida. Hiyo ni kwa sababu inawanyima watu uhuru wao wa faragha.

 • Windows 10: Kuna Nini Microsoft Hawatuambii na Kwanini Inashida Sana?

  07/01/2023 Duración: 25min

  Watumiaji wengi wa Windows 10 wamekutana na errors zilizopelekea wao kushindwa kufanya kazi. Mara nyingi hii inatokea baada ya kufanya update na kusalimiwa na BSOD (Blue Screen of Death). Kuna nini Microsoft wameshindwa kuboresha kwenye Windows 10 mpaka inakuwa hivi?

 • HABARITECH: Tecno Phantom X2

  28/12/2022 Duración: 21min

  Flagship ya kwanza kutoka Tecno ikiwa na processor ya uwezo mkubwa na camera nzuri ya kushindanishwa na iPhone 14.

 • Kuachana na Simu Yangu

  08/04/2022 Duración: 07min

  Barua hii ya kuachana na simu yako imeandikwa kwa lugha ya kiingereza na Catherine Price katika kitabu chake cha "How to break up with your Phone". Imetafsiriwa na kusomwa na Charles Venny wa HabariTech