Sinopsis
Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali.
Episodios
-
Jukwaa La Michezo: Cheptegei aishindia Uganda medali ya kwanza Olimpiki ya Paris
03/08/2024 Duración: 23minJoshua Cheptegei ashinda medali ya dhahabu kwenye mbio za mita 10,000 huku Malkia Strikers ikibanduliwa mashindanoni. Morocco na Misri zafuzu nusu fainali huku waafrika kwenye uogeleaji wakifanya vibaya. Pia tutakufahamisha matokeo ya judo, basketboli, kuendesha basikeli na jedwali la medali ambapo Uchina inazidi kuongoza jedwali hilo
-
Paris Olimpiki: Ufaransa yashinda dhahabu ya raga, Kenya ikimaliza nambari tisa
28/07/2024 Duración: 23minTuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa matokeo ya Olimpiki na mjadala kuhusu wanariadha wanaotarajiwa kung'ara kwenye Olimpiki wiki ijayo riadha zitakapoanza pamoja na matokeo ya Toyota Cup Yanga ikiilaza Kaizer Chiefs huku George Russel akishinda mkondo wa Belgian GP kwenye mashindano ya langalanga.
-
Olimpiki ya Paris: Mambo muhimu ya kujua kuhusu mashindano ya mwaka huu
20/07/2024 Duración: 17minTuliyokuandalia ni pamoja na mambo muhimu unahitaji kujua kuhusu Olimpiki ya mwaka huu kabla ya kuanza, uchambuzi wa fainali ya CECAFA Kagame Cup kati ya APR ya Rwanda na Red Arrows ya Zambia, tetesi za uhamisho Afrika Mashariki n aUlaya pamoja na matokeo ya Tour de France ikielekea ukingoni huku kocha wa Uingereza Gareth Southgate akijiuzulu kuifunza timu ya taifa ya wanaume.
-
Timu ya Kenya yaanza kuwasili Miramas, Ufaransa tayari kwa Olimpiki
13/07/2024 Duración: 23minTuliyokuandalia ni pamoja na droo ya hatua ya awali kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika msimu ujao, matokeo ya Monaco Diamond League, Team Kenya yaanza kuwasili Ufaransa tayari kwa Olimpiki, matokeo ya CECAFA Kagame Cup na tetes iza uhamisho pamoja na uchambuzi wa fainali ya EURO, Copa America na fainali za tenisi kwenye Wimbledon.