Gurudumu La Uchumi

Informações:

Sinopsis

Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .

Episodios

  • Viongozi wa dunia wajadili malengo endelevu ya umoja wa Mataifa

    05/10/2023 Duración: 09min

    Mwezi uliopita, viongozi wa dunia walikutana jijini New York, Marekani katika mkutano wa 78 wa baraza la umoja wa Mataifa, ambapo walijadiliana masuala mbalimbali ikiwemo usalama wa dunia na ukuaji wa uchumi pamoja na mikakati ya kufikia ajenda ya mwaka 2030 na haja ya kuongeza kasi kutekeleza malengo 17 endelevu. Kuzungumzia yaliyojiri, mtayarishaji wa makala haya alimualika Ebenezer Suleiman Mathew Ikomba, balozi wa vijana wa Tanzania kwenye umoja wa Mataifa. Katika mijadala mingi, vijana walitajwa kuwa sehemu kubwa ya nguvu kazi ya dunia na kwamba kupitia ubunifu, uwajibikaji na harakati za kuhamasisha nchi kufikia malengo endelevu, basi dunia itakuwa sehemu salama. Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili inaangazia yaliyotokana kwenye mkutano huo na namna gani vijana wanaweza kushiriki katika ujenzi wa dunia salama na yenye amani ambayo itachochea maendeleo na ukuaji wa uchumi. 

  • Tatizo la uhaba wa dola ya Marekani kwenye nchi za Afrika Mashariki

    22/09/2023 Duración: 09min

    Katika Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, mtayarishaji wa makala haya amezungumza na Profesa Wetengere Kitojo, mtaalamu wa masuala ya uchumi akiwa Tanzania, ambapo wanaangazia kuhusu tatizo la uhaba wa dola ya Marekani kwenye nchi za Afrika Mashariki. 

  • Biashara ya madini yaimarika nchini DRC

    07/09/2023 Duración: 09min

    Wiki hii tunaangazia huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambako kunaripotiwa ongezeko kubwa la uzalishaji wa madini ya shaba na kobalt katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Takwimu kutoka sekta ya madini, zinaonesha kuwa uzalishaji wa kobalt imeongezeka na kufikia zaidi ya Tani Laki moja, baada ya serikali kuwekeza asilimia 43 ya bajeti yake ya taifa kwenye sekta hiyo. Kwenye Makala haya, mwandishi wetu wa Lubumbashi Denise Maheho, amezungumza na watafiti wa madini na mashirika ya kiraia, katika eneo la Katanga.

  • Nguo za mitumba zapigwa marufuku nchini Uganda

    01/09/2023 Duración: 09min

    Serikali ya Uganda imepiga marufuku uingizwaji na uuzwaji wa nguo kukuu maarufu kama mitumba nchini humo. Rais Yoweri Museveni anasema, hatua hiyo itasaidia kukusa viwanda vya ndani vya nguo na kuunda ajira hasa kwa vijana. Mwandishi wetu wa Kampala Kenneth Lukwago anatueleza zaidi.

página 2 de 2