Habari Za Un
10 OKTOBA 2024
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:11:20
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika malengo ya maendeleo endelevu. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwema za Lebanon, afya ya akili na ripoti ya UNICEF kuhusu ukatili wa kingono. Katika kujifunza Kiswahili tunakuletea uchambuzi wa methali.Nchini Lebanon ujumbe wa jeshi la Umoja wa Mataifa la mpito nchini humo, UNIFIL, unasema mapigano kati ya jeshi la Israeli, IDF, na wanamgambo wa Hezbollah kusini mwa Lebanon yamekuwa na madhara kwa ujumbe huo kwani makao yake makuu huko Naqourra na maeneo ya karibu yameshambuliwa mara kwa mara tangu kuanza kwa mapigano kati ya pande hizo mbili.Leo ni siku ya afya ya akili duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake amesisitiza udharura wa kupatia kipaumbele afya ya akili pahala pa kazi.Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linasema zaidi ya wasichana na wanawake milioni 370 walioko hai hii leo, walikumbwa na ukatili wa kingono wakati wa utoto wao, yaani kabla ya