Sinopsis
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Episodios
-
Zanzibar tumetekeleza kwa vitendo azimio la Beijing: Waziri Riziki Pembe
21/03/2025 Duración: 05minWakati mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani CSW69 ukifikia ukingoni mshiriki kutoka Zanzibar Tanzania ameweleza Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili kwamba Zanzibar imepiga hatua kubwa katika usawa wa kijinsia na utekelezaji kwa vitendo matakwa ya Azimio la Beijing la usawa wa kijinsia na hatua. Je wametekeleza vipi na hatua gani walizopiga? Ungana nao katika mahojiano haya.
-
Ukiwekeza kiuchumi kwa mwanamke basi umewekeza katika jamii: Janet Mbene mshiriki CSW69
21/03/2025 Duración: 05minMkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani CSW69 unakunja jamvi leo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani baada ya mjadala wa wiki mbili kutathimini hatua zilizopigwa na changamoto zilizosalia miaka 30 baada ya azimio la Beijing la usawa wa kijinsia nah atua za utekelezaji. Flora Nducha amebahatika kuzungumza na mmoja wa wakishiri wa mkutano huo kutoka asasi za kiraia nchini Tanzania
-
IFAD yawaepusha vijana wa kike 5 na kazi za ndani na kuwajengea stadi za kilimo biashara Senegal
21/03/2025 Duración: 02minTukiwa bado ndani ya mwezi wa Machi, unaotambuliwa kuwa ni mwezi wa wanawake tunakwenda nchini Senegal ambako huko wasichana waliokuwa wakifanya kazi za ndani, wamewezeshwa na Umoja wa Mataifa na sasa ni wakulima na wanatumia stadi za upigaji na utengenezaji video za mtandaoni kuelimisha jamii kuhusu kilimo chenye tija. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
-
21 MACHI 2025
21/03/2025 Duración: 10minHii leo jaridani tunaangazia mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, CSW69 unafikia tamati hii leo Machi 21 hapa katika makao makuu, na wakulima wanawake nchini Senegal. Mashinani inatupeleka nchini Tanzania kumulika mradi wa maji.Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, CSW69 unafikia tamati hii leo Machi 21 hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Bi. Gertrude Mongella, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano wa 4 wa Kimataifa wa wanawake maarufu kama Mkutano wa Beijing uliofanyika mnamo mwaka 1995, hivi tunavyozungumza, pamoja na umri wake mkubwa ameshirikia karibia vikao vyote vya mkutano huu wa CSW69 ambao pia ulikuwa unaangazia utekelezaji wa maazimio yaliyowekwa miaka 30 iliyopita chini yake mama Mongella.Tukiwa bado ndani ya mwezi wa Machi, unaotambuliwa kuwa ni mwezi wa wanawake tunakwenda nchini Senegal ambako huko wasichana waliokuwa wakifanya kazi za ndani, wamewezeshwa na Umoja wa Mataifa na sasa ni wakulima na wanatumia stadi za upigaji na ut
-
Wanaume 'wapenzi wetu' msiwe na hofu na sisi - Bi. Gertrude Mongella
21/03/2025 Duración: 01minMkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, CSW69 unafikia tamati hii leo Machi 21 hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.Bi. Gertrude Mongella, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano wa 4 wa Kimataifa wa wanawake maarufu kama Mkutano wa Beijing uliofanyika mnamo mwaka 1995, hivi tunavyozungumza, pamoja na umri wake mkubwa ameshirikia karibia vikao vyote vya mkutano huu wa CSW69 ambao pia ulikuwa unaangazia utekelezaji wa maazimio yaliyowekwa miaka 30 iliyopita chini yake mama Mongella.Nilipokutana naye nimemuuliza swali hili la kichokozi.Mazungumzo zaidi kati yangu na Mama Gertrude Mongella yatakujia katika vipindi vyetu vijavyo hivi karibuni.
-
Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi wa maneno "Ashiraf, Janabi, gayagaya, kiti cha marimba na kiti cha msaji"
20/03/2025 Duración: 59sKatika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya maneno “Ashiraf, Janabi, gayagaya, kiti cha marimba na kiti cha msaji”
-
20 MACHI 2025
20/03/2025 Duración: 12minHii leo jaridani katika mada kwa kina tunajikita katika mkutano CSW69 ambao umebakiza siku moja tu, kesho Machi 21 unakunja jamvi, na tunamsikia Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Tanzania, Waziri Riziki Pembe kutoka Zanzibar na Profesa Smile Dzisi, Mkugenzi wa Shirika la “I believe Global” kutoka Ghana.Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi amesema kukata ufadhili kwa mashirika yanayotoa huduma za kibinadamu kunasababisha janga la uwajibikaji. Kupitia taarifa iliyotolewa leo Geneva, Uswisi na UNHCR, Bwana Grandi amesema kukata ufadhili kunaweka hatarini maisha ya mamilioni ya watu na madhara yake kwa watu wanaokimbia majanga, yatakuwa makubwa zaidi na yataonekana wazi ikiwemo wanawake na watoto wa kike kukosa huduma zitokanazo na kubakwa.Leo ni siku ya furaha duniani maudhui yakimulika umuhimu wa watu kusaidiana na kujaliana katika masuala mbalimbali ikiwemo chakula. Ripoti mpya ya wadau wa UN iliyozinduliwa leo imeonesha kuwa nchi ye
-
Lengo langu ni kuona wasichana wadogo wanashiriki kwa wingi CSW - Zahra Salehe ICCAO
19/03/2025 Duración: 03minKatika makala Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa anazungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la ICCAO kutoka Tanzania, Zahra Salehe, mshiriki mwingine kutoka Tanzania anayehudhuria mkutano wa 69 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW69 unaoendelea hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, jijini New York Marekani.
-
Haki za wanawake na wasichana lazima zizingatiwe na zipewe kipaumbele - Ochieng CSW69
19/03/2025 Duración: 02minMkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW69 unaendelea kujadili mafanikio yaliyopatikana na nini kifanyike zaidi kutimiza lengo la miaka 30 iliyopita la azimio la Beijing. Mwanzilishi na mkurugenzi mkuu wa shirika la slums foundation lililoko jijiniNairobi, Kenya naye anashiriki mkutano huu wa CSW69 na ameueleza Sharon Jebichii wa Idhaa hii kilichomleta hapa, matarajio yake na ushauri kwa wasichana na wanawake.
-
19 NACHI 2025
19/03/2025 Duración: 09minHii leo jaridani tunaangazia madhara ya mabadiliko ya tabianchi yanayosababishwa na binadamu, na yaliyojiri hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa mkutano wa 69 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW69.Madhara ya mabadiliko ya tabianchi yanayosababishwa na binadamu yameongezeka kwa viwango vya kutisha mwaka 2024, na baadhi ya athari hasi zinaweza kuwa zisizoweza kurekebishwa kwa karne nyingi – kama si milenia, imesema ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa, (WMO).Tukirejea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW69 unaendelea kujadili mafanikio yaliyopatikana na nini kifanyike zaidi kutimiza lengo la miaka 30 iliyopita la azimio la Beijing. Mwanzilishi na mkurugenzi mkuu wa shirika la slums foundation lililoko jijiniNairobi, Kenya naye anashiriki mkutano huu wa CSW69 na ameueleza Sharon Jebichii wa Idhaa hii kilichomleta hapa, matarajio yake na ushauri kwa wasichana na wanawake..Makala Flora Nducha wa Idhaa hii anazun
-
WMO: Joto likizidi kuongezeka duniani, mwaka 2024 wathibitishwa kuwa ulikuwa wa joto zaidi
19/03/2025 Duración: 01minMadhara ya mabadiliko ya tabianchi yanayosababishwa na binadamu yameongezeka kwa viwango vya kutisha mwaka 2024, na baadhi ya athari hasi zinaweza kuwa zisizoweza kurekebishwa kwa karne nyingi – kama si milenia, imesema ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa, (WMO). Anold Kayanda na maelezo zaidi.
-
18 MACHI 2025
18/03/2025 Duración: 11minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kumulika elimu ya mtoto wa kike kama moja ya nguzo muhimu katika jamii ukizingatia malengo endelevu ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa.Pia tunakuletea muhtasari wa habari na sauti za mashinani.Viongozi wa Umoja wa Mataifa leo wamelaani vikali mashambulizi ya anga ya Israel huko Ukanda wa Gaza na kutoa wito kwa kusitisha uhasama mara moja. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonesha mshtuko na wasiwasi mkubwa kuhusu mashambulizi hayo akitoa wito kwa pande zote kuheshimu usitishaji mapigano, kurejesha misaada ya kibinadamu bila vikwazo, na kuhakikisha kuachiliwa mara moja na bila masharti kwa mateka waliobaki.Ghasia zinazoendelea katika kaunti za Nasir, Ulang, na Baliet, Jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini zimeathiri vibaya jamii za eneo hilo na shughuli za kibinadamu, na kusababisha watu takriban 50,000 kukimbia makazi yao tangu mwishoni mwa mwezi Februari amesema Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini S
-
Melvin Wajir: Ushiriki wa wanawake unapaswa kuwa mezani na sio katika menyu
17/03/2025 Duración: 03minIli kufanikisha lengo la usawa wa kijinsia Umoja wa Mataifa unasisitiza ushiriki wa wanaume katika mchakato hasa kwa kuzingatia kuwa mfumo dume miaka nenda miaka rudi umekuwa kikwazo cha kufikia lengo hilo, Flora Nducha wa idhaa hii amebahatika kuzungumza na mmoja wa wanaume wanaoshiriki mkutano huo kusikia maoni yake.
-
UNCTAD: Wekeni wazi mikataba ya madeni mnayokopa ili kujenga imani kwa wananchi
17/03/2025 Duración: 01minMkutano wa 14 wa Kimataifa wa Usimamizi wa madeni umeanza rasmi hii leo huko Geneva Uswisi ambapo kubwa linalojadiliwa ni namna ya kuhakikisha wakati serikali zikipambana kulipa madeni hazidumazi maendeleo. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Assumpta Massoi
-
17 MACHI 2025
17/03/2025 Duración: 11minHii leo jaridani tunaangazia madeni katika nchi zenye mapato ya chini na ujumbe wa washiriki wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani CSW69 hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa.Mkutano wa 14 wa Kimataifa wa Usimamizi wa madeni umeanza rasmi hii leo huko Geneva Uswisi ambapo kubwa linalojadiliwa ni namna ya kuhakikisha wakati serikali zikipambana kulipa madeni hazidumazi maendeleo.Akijibu swali la kwa nini pamoja na ongezeko na idadi ya wanawake katika ngazi za uamuzi nchini Tanzania lakini bado kuna changamoto zinazoukabili usawa wa kijinsia, Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu anayehudhuria mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake, CSW69 jijini New York, Marekani kupitia mahojiano maalumu na Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Umoja wa Mataifa, anaeleza kuwa mabadiliko chanya katika jamii hayaji kwa kutumia mabavu.Makala pia inatubakisha hapa Umoja wa Mataifa kwenye mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani CSW69.
-
Mabadiliko chanya katika jamii yanakuja kwa kueleweshana - Dkt. Gwajima
17/03/2025 Duración: 02minWaziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Waziri, Dkt. Dorothy Gwajima, ni mmoja wa wanaohudhuria mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake, CSW69 hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Anold Kayanda wa Idhaa hii amekutana naye na miongoni mwa mambo mengi amemuuliza ni kwa nini pamoja na ongezeko na idadi ya wanawake katika ngazi za uamuzi nchini Tanzania lakini bado kuna changamoto nyingi zinazoukabili usawa wa kijinsia nchini humo?
-
Azimio la Beijing limeleta manufaa kwa wanawake Côte d'Ivoire - Francine
14/03/2025 Duración: 04minKutana na Francine Aka Epse Akaanghui Rais wa Chama cha wanasheria wanawake nchini Côte d'Ivoire huko Afrika Magharibi. Yeye anashiriki mkutano wa 69 wa Hali ya Wanawake duniani, CSW69 akisema taifa lake lina mengi ya kujivunia wakati huu wa kuadhimisha miaka 30 tangu kupitishwa kwa Azimio la Beijing na Jukwaa la Utekelezaji. Francine amezungumza na Assumpta Massoi katika makala hii.
-
14 MACHI 2025
14/03/2025 Duración: 09minHii leo jaridani tunaangazia ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres huko Bangladesh, na yaliyojiri hapa makao makuu katika mkutano wa CSW69. Makala na mashinani tunasalia hapa hapa makao makuu, kulikoni?Akiwa ziarani katika kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani, Cox’s Bazar, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo Machi 14 ameonya kuhusu hali mbaya ya kibinadamu inayowakabili zaidi ya wakimbizi milioni moja wa Rohingya nchini Bangladesh.Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW69 unaendelea kujadili mafanikio yaliyopatikana na nini kifanyike zaidi kutimiza lengo la miaka 30 iliyopita la azimio la Beijing. Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano huo wa mwaka 1995 yuko kwenye mkutano huu CSW69 Flora Nducha wa Idhaa alipata fursa ya kuuliza nini tathimini yake ya utekelezaji wa azimio la Beijing na kinachohitajika zaidi kutimiza lengo la azimio hilo.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC hii leo Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda ama
-
Katibu Mkuu afuturu na wakimbizi wa Rohingya nchini Bangladesh
14/03/2025 Duración: 01minLeo Ijumaa ikiwa ni siku ya 11 ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amefuturu na wakimbizi wa Rohingya walioko kwenye kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani, Cox Baazar nchini Bangladesh kuonesha mshikamano na wakimbizi na wenyeji wanaowahifadhi. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
-
Getrude Mongella: Ukilinganisha na tulikotoka tumepiga hatua lakini safari bad oni ndefu
14/03/2025 Duración: 01minTukirejea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, mkutano wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW69 unaendelea kujadili mafanikio yaliyopatikana na nini kifanyike zaidi kutimiza lengo la miaka 30 iliyopita la azimio la Beijing. Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Mkutano huo wa mwaka 1995 yuko kwenye mkutano huu CSW69 Flora Nducha wa Idhaa alipata fursa ya kuuliza nini tathimini yake ya utekelezaji wa azimio la Beijing na kinachohitajika zaidi kutimiza lengo la azimio hilo.

Únete Ahora
- Acceso ilimitado a todo el contenido de la plataforma.
- Más de 30 mil títulos, incluidos audiolibros, podcasts, series y documentales.
- Narración de audiolibros por profesionales, incluidos actores, locutores e incluso los propios autores.