Sinopsis
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Episodios
-
19 MEI 2025
19/05/2025 Duración: 11minHii leo jaridani tunaangazia masuala ya afya, na wakimbizi wa Syria wanaorejea nchini mwao. Makala tukwenda nchini Kenya kumulika ufukaji wa nyuki, na mashinani tunakuletea ujumbe wa Katibu Mkuu wa IMO kuhusu Siku ya Kimataifa ya wanawake mabaharia.Wajumbe kutoka kote duniani wamekusanyika mjini Geneva, Uswisi, kwa ajili ya Mkutano wa 78 wa Baraza la Afya Duniani (WHA78) unaofanyika kuanzia leo Mei 19 hadi 27 Mei mwaka huu.Tangu kuangushwa kwa utawala wa aliyekuwa Rais wa Syria Bashar al Assad aliyekuwa madarakani kwa zaidi ya muongo mmoja, wananchi wa Syria wamekuwa wakimiminika kurejea nchini mwao ambapo takwimu za sasa zinaonesha zaidi ya Wasyria 500,000 wamerejea kutoka nchi jirani. Mmoja wa waliorejea ni Babu Jassim na Leah Mushi anatuletea simulizi yake.Katika makala tunaelekea Kajiado nchini Kenya, ambako juhudi za utunzaji mazingira kupitia mradi wa ufugaji wa nyuki unaofadhiliwa na shirika la misaada la Marekani USAID kwa kushirikiana na idara ya misitu ya Kenya KFS hazichangii tu katika kukuza uchum
-
WHO: Mkutano wa 78 wa Baraza la Afaya Duniani umeng’oa nanga Geneva
19/05/2025 Duración: 02minWajumbe kutoka kote duniani wamekusanyika mjini Geneva, Uswisi, kwa ajili ya Mkutano wa 78 wa Baraza la Afya Duniani (WHA78) unaofanyika kuanzia leo Mei 19 hadi 27 Mei mwaka huu. Kaulimbiu ya mkutano wa mwaka huu ni “Ulimwengu Mmoja kwa Afya” inaakisi dhamira ya pamoja ya kujenga mfumo wa afya wa kimataifa ulio imara, jumuishi na thabiti. Flora Nducha amefuatilia na hapa anatupasha zaidi
-
UN Women Tanzania yawawezesha wanawake wenye ulemavu kujiinua kiuchumi
16/05/2025 Duración: 05minShirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN WOMEN nchini Tanzania linaendesha mradi wa wanawake na uongozi chini ya ufadhili wa Finland mradi unaolenga kuwawezesha wanawake wenye ulemavu kujikwamua kiuchumi na pia kushiriki katika ngazi za uongozi katika maeneo yao.Kupitia makala hii Leah Mushi anatukutanisha na wanawake wawili walionufaika na mradi huo wa UN WOMEN na wanaeleza namna jamii zao zilivyokuwa kabla na baada ya kupatiwa elimu ya masuala mbalimbali yahusuyo watu wenye ulemavu.
-
FAO: Mikakati sahihi ya kilimo imeepusha mamilioni kutumbukia kwenye baa la njaa
16/05/2025 Duración: 02minUkosefu wa uhakika wa kupata chakula na utapiamlo kwa watoto uliongezeka kwa mwaka wa sita mfululizo mwaka 2024, na kuwatumbukiza mamilioni ya watu karibu na baa la njaa, huku wengine wakiepuka kutokana na misaada ya kimkakati. Imesema Ripoti ya Kimataifa kuhusu Janga la Chakula (GRFC) iliyotolewa leo huko Roma, Italia na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO. Flora Nducha anakutaarifu kwa muhtasari.
-
16 MEI 2025
16/05/2025 Duración: 12minHii leo jaridani tunaangazia uhakika wa chakula, na takwimu za afya za janga la COVID-19 kusababisha vifo, muda wa kuishi na hali ya afya na ustawi kwa ujumla. Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani nchini DRC, kulikoni?Ukosefu wa uhakika wa kupata chakula na utapiamlo kwa watoto uliongezeka kwa mwaka wa sita mfululizo mwaka 2024, na kuwatumbukiza mamilioni ya watu karibu na baa la njaa, huku wengine wakiepuka kutokana na misaada ya kimkakati. Imesema Ripoti ya Kimataifa kuhusu Janga la Chakula (GRFC) iliyotolewa leo huko Roma, Italia na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO.Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) ya takwimu za afya duniani iliyochapishwa jana Mei 15 ikionesha athari kubwa zaidi za kiafya zilizosababishwa na janga la COVID-19 kuhusu vifo, muda wa kuishi na hali ya afya na ustawi kwa ujumla, imeweka wazi kuwa katika kipindi cha miaka miwili pekee, kati ya mwaka 2019 na 2021, matarajio ya kuishi yalipungua kwa mwaka mmoja na miezi nane ikiwa ni
-
WHO: Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanachangia nusu ya vifo chini ya umri wa miaka 70
16/05/2025 Duración: 02minRipoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) ya takwimu za afya duniani iliyochapishwa jana Mei 15 ikionesha athari kubwa zaidi za kiafya zilizosababishwa na janga la COVID-19 kuhusu vifo, muda wa kuishi na hali ya afya na ustawi kwa ujumla, imeweka wazi kuwa katika kipindi cha miaka miwili pekee, kati ya mwaka 2019 na 2021, matarajio ya kuishi yalipungua kwa mwaka mmoja na miezi nane ikiwa ni maporomoko makubwa zaidi katika historia ya hivi karibuni hali iliyobatilisha mafanikio ya afya yaliyopatikana kwa muongo mmoja.
-
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno "KIANGO."
15/05/2025 Duración: 52sKatika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno "KIANGO."
-
15 MEI 2025
15/05/2025 Duración: 09minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturejesha katika mkutano wa CSW68 kumsikia Christina Kamili Ruhinda, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Mashirika yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria nchini Tanzania, TANLAP. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno la wiki.Wakati dunia ikiadhimisha miaka 77 tangu Nakba ambapo zaidi ya wapalestina 700,000 walifurushwa kutoka vijiji na miji yao mwaka 1948, shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa Wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limetoa onyo kali kuhusu sura mpya ya mateso na ufurushwaji wa lazima uonaoendele Gaza.Akiwa na wasiwasi kutokana na ripoti za kuaminika kwamba wakimbizi wa Rohingya kutoka Myanmar walilazimishwa kushuka kutoka kwenye meli ya jeshi la wanamaji la India na kutoswa katika bahari ya Andaman wiki iliyopita, Mtaalamu wa UN wa Haki za Binadamu kuhusu wakimbizi wa Myanmar, ameanzisha uchunguzi kuhusu kitendo hicho alichoeleza kuwa ni cha kushangaza na kisichokubalika.Na baada ya muda mrefu kuonekana kama mchangiaji mkubwa wa uto
-
Wataalamu huru walaani mashambulizi ya kikatili dhidi ya wanawake na wasichana - Sudan
14/05/2025 Duración: 01minWataalamu huru wa haki za binadamu, leo Mei 14 wamekemea vikali ukiukwaji mkubwa na wa kimfumo dhidi ya wanawake na wasichana nchini Sudan ukiwemo ukatili wa kingono unaohusiana na vita, utekaji nyara, na mauaji, ambayo mengi yameripotiwa kufanywa na kundi la kijeshi la Rapid Support Forces (RSF). Anold Kayanda na taarifa zaidi.
-
Nyumba yetu ilivamiwa na tulilazimika kukimbia hadi hapa Burundi – Mkimbizi Charles
14/05/2025 Duración: 04minMapigano yanayoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, yamesababisha zaidi ya watu 70,000 kukimbia makazi yao na kuvuka mpaka kuingia nchi jirani ya Burundi wakitafuta usalama.
-
14 MEI 2025
14/05/2025 Duración: 10minHii leo jaridani tunaangazia haki za wanawake na wasichana nchini Sudan na hali ya kina mama na wanawake wajawazitio katika ukanda wa Gaza. Makala tukwenda nchini Burundi na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Wataalamu huru wa haki za binadamu, leo Mei 14 wamekemea vikali ukiukwaji mkubwa na wa kimfumo dhidi ya wanawake na wasichana nchini Sudan ukiwemo ukatili wa kingono unaohusiana na vita, utekaji nyara, na mauaji, ambayo mengi yameripotiwa kufanywa na kundi la kijeshi la Rapid Support Forces (RSF).Huko Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli, wanawake na wasichana wakiwemo wanawake wajawazito na wale waliojifungua, wamelazimika kukimbia makazi yao na wanaishi katika mazingira hatarishi bila huduma za msingi za kiafya. Sharon Jebichii anaangazia simulizi ya mama mmoja, mkazi wa kambi ya wakimbizi ya Jabalia, Kaskazini mwa Gaza, ambaye alijifungua akiwa amekimbia vita,na sasa anahangaika kumtunza binti yake mchanga.Katika makala Assumpta Massoi kwa makala hiyo na zaidi ya yote shirika la Umoja wa M
-
Akina mama wakimbizi katika ukanda wa Gaza wanataabika bila huduma za afya
14/05/2025 Duración: 02minHuko Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli, wanawake na wasichana wakiwemo wanawake wajawazito na wale waliojifungua, wamelazimika kukimbia makazi yao na wanaishi katika mazingira hatarishi bila huduma za msingi za kiafya. Sharon Jebichii anaangazia simulizi ya mama mmoja, mkazi wa kambi ya wakimbizi ya Jabalia, Kaskazini mwa Gaza, ambaye alijifungua akiwa amekimbia vita,na sasa anahangaika kumtunza binti yake mchanga.
-
13 MEI 2025
13/05/2025 Duración: 11minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika lengo namba moja la Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDG1 la kutokomeza umaskini na inatupeleka nchini Tanzania ambako Umoja wa Mataifa umeona bora kusaidia wafugaji kuku kuondokana na umaskini.Katika mkutano wa ngazi ya mawaziri kuhusu mustakabali wa ulinzi wa amani unaofanyika leo mjini Berlin Ujerumani Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameeleza vipaumbele vitatu vya msingi katika mageuzi ya ulinzi wa amani kwa muktadha wa dunia inayobadilika kwa kasi.Mashariki ya Kati leo shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limeonya kuhusu vifo vya watoto kutokana na utapiamlo Gaza, sababu kubwa ikiwa ni kuendelea kukosekana kwa msaada wa kibinadamu unaojumuisha lishe maalum kwa watoto.Wakati mahitaji ya kibinadamu yakizidi kuongezeka duniani watu milioni 308 katika nchi 73 wakihitaji msaada wa dharura , Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women limeonya kuwa wanawake na wasichana ndio wanaoathirika zaidi wa migogoro, wakik
-
Bi. Joy :Teknolojia inatatua changamoto za kijamii - Wasichana katika TEHAMA
12/05/2025 Duración: 03minKwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO, sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano TEHAMA, au ICT inaendelea kutawala na kuunda fursa mpya, lakini wanawake bado wanakumbana na changamoto kubwa ya upungufu wa uwakilishi. Hata hivyo, wanawake wanavuka mipaka na sasa Bi. Joy, msichana kutoka Nairobi Kenya, ambaye ni mtaalamu katika teknolojia ya kidijitali, amekalia nafasi muhimu katika kubadili mtindo wa maisha kupitia elimu ya ICT. Katika mahojiano na washirika wetu Radio Domus, alizungumzia umuhimu wa kuhamasisha wasichana kujiunga na masomo ya teknolojia ili kutengeneza mustakabali mpya wa kidijitali, na kubadili dunia kwa njia ya kidigitali na usawa. Sharon Jebichii na Makala zaidi
-
12 MEI 2025
12/05/2025 Duración: 11minHali mbaya ya hewa na mabadiliko ya tabianchi vyaliacha hoi bara la Afrika yaonya WMO.WHO yahaha kukabiliana na kipindupindu Angola.Makala Sharon Jebichii anatupeleka nchini Kenya, kumulika masuala ya wasichana katika ICT.Mashinani leo inaangazia ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa wiki ya usalama barababarni.
-
WHO na vita dhidi ya kipundupindu Angola.
12/05/2025 Duración: 02minTangu Januari mwaka huu 2025 nchini Angola, ugonjwa wa kipindupindu umesambaa katika majimbo 17 kati ya 21 ya nchi hiyo. Mlipuko huu tayari umesababisha karibu vifo 600 linaeleza Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO. António Catunda, ni Msimamizi wa Uhamasishaji wa Afya katika kituo cha afya cha Sambizanga jimboni Luanda unakopatikana mji Mkuu wa Angola. Kupitia video iliyoandaliwa na WHO, anaielezea hali ilivyo.
-
Hali mbaya ya hewa na mabadiliko ya tabianchi vyaliacha hoi bara la Afrika yaonya WMO.
12/05/2025 Duración: 02minRipoti mpya kuhusu “Hali ya Hewa Afrika 2024” iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani WMO imeonya kwamba muongo wa joto zaidi kuwahi kushuhudiwa Afrika umeleta madhara makubwa kwa bara hilo. Evarist Mapesa na taarifa zaidi
-
Chokoleti itengenezwayo Uganda yavuka mpaka na mabara -UNCTAD
09/05/2025 Duración: 03minKutoka kakao ghafi huko Bundibugyo, magharibi mwa Uganda hadi Kampala mji mkuu wa kibiashara wa taifa hilo la Afrika Mashariki ndiko kunapatikana kiwanda cha kutengeneza chokoleti cha Equator kinachomilikiwa na Barbara Gonget na mume wake Gustav. Awali wazo la biashara hii lilionekana kutokuwa na mashiko. Ingawa hivyo baada ya ITC, ambacho ni Kituo cha Kimataifa ha Biashara kilicho chini ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo, UNCTAD pamoja na wadau wao kuweka usaidizi wao, hali imebadilika na sasa biashara inavuka sio tu mipaka bali mabara. Wawili hao Kwa kuchanganya mbinu za hali ya juu, zinazojali jamii, na ufundi wa kitaalamu, wanabadili taswira ya uzalishaji wa chokoleti nchini humo.Je wamefanya nini? Assumpta Massoi anafafanua zaidi kwenye makala hii iliyofanikishwa na ITC.
-
Mashirika ya UN yakemea mpango wa Israel kutumia misaada kama mtego - Gaza
09/05/2025 Duración: 01minMpango wa Israel wa kuchukua udhibiti wa misaada ya dharura huko Gaza utaweka maisha ya raia hatarini na kusababisha ufurushwaji Mkubwa wa watu huku ikitumia misaada kama mtego, walisema leo wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa. Anold Kayanda anafafanua zaidi
-
09 MEI 2025
09/05/2025 Duración: 09minKatika Jarida la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea-Gaza: Mashirika ya Umoja wa Mataifa leo yakemea mpango wa Israel kutumia misaada kama mtego-Mradi wa HOTIGRO wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP nchini Tanzania wainua wakulima wa mboga na matunda -Makala leo inatupeleka Uganda kumulika kiwanda cha kutengeneza chokoleti-Na mashinani tunabisha hodi Kenya kunakofanyika mkutano wa UNESCO kuhusu urithi wa utamaduni wa Afrika

Únete Ahora
- Acceso ilimitado a todo el contenido de la plataforma.
- Más de 30 mil títulos, incluidos audiolibros, podcasts, series y documentales.
- Narración de audiolibros por profesionales, incluidos actores, locutores e incluso los propios autores.