Habari Za Un
Mwaka 1 wa vita Mashariki ya Kati: Ni wakati wa amani Gaza, asema Guterres
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 0:02:14
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Leo ni mwaka mmoja tangu vita ianze huko Gaza, Mashariki ya Kati baada ya wanamgambo wa kipalestina, Hamas kushambulia Israeli na kuua waisraeli 1250 pamoja na wageni, kisha Israeli kujibu mashambulizi yaliyoripotiwa kuua hadi sasa zaidi ya wapalestina 41,000 ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pamoja na wakuu wa mashirika mbali mbali ya chombo hicho wametoa wito kutaka kukoma kwa vita hiyo. Assumpta Massoi na maelezo zaidi. Antonio Guterres huyu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wake kwa njia ya video leo ikiwa in mwaka mmoja, anasema hii ni siku kwa jamii ya kimataifa kurejelea tena kwa sauti kubwa zaidi kulaani kwetu kwa vitendo vya kuchukiza vya Hamas ikiwemo utekaji nyara wa siku ile.Hamas waliteka nyara zaidi ya watu 250. Guterres amesema katika kipindi cha mwaka mmoja amezungumza na familia ambazo ndugu zao wanashikiliwa mateka hadi sasa. Amezungumzia pia machungu yaliyoibuka baada ya vita kuanza. Sasa anasema ni wakati wa kuachilia huru mateka. Wakati wa kunyamazisha bunduki.