Habari Za Un

UNESCO: Tunapaswa kuthamini sauti za walimu kote duniani

Informações:

Sinopsis

Washiriki wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Walimu ililofanyika leo Oktoba 4 katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jijini Paris, Ufaransa  wamesisitiza wito wa kuthamini mawazo ya walimu katika kuboresha elimu ya ulimwengu. Kama tunavyofahamu, siku yenyewe ya Kimataifa ya Walimu ni kesho Oktoba 5 kama ilivyo ada ya kila mwaka lakini katika makao makuu ya UNESCO hapa Paris Ufaransa, maadhimisho yamefanyika leo kuelekea mkesha wa siku hii muhimu kwa elimu ya ulimwengu.Miongoni mwa waliozungumza ni Mkurugenzi Msaidizi Mkuu wa Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi Stefania Giannini, ambaye ameitumia nafasi hii kusisitiza kauli mbiu ya mwaka huu ambayo ni 'Kutambua sauti za walimu.'Anasema, “walimu ni uti wa mgongo wa mifumo ya elimu na mawakala wakuu wa mabadiliko ya kubuni sera za elimu na kufanikisha SDGs. Tunapaswa kuthamini sauti za walimu; hili ndilo lengo kuu la Siku ya Kimataifa ya Walim