Siha Njema

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 4:01:50
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.

Episodios

  • Ubunifu kutatua changamoto za miundombinu kwenye usafi na maji taka

    24/09/2024 Duración: 10min

    Mashirika ya nchini Kenya  kwa ushirikiano na serikali za kaunti ,yamezindua  mfumo mpya na wa kisasa wa vyoo bunifu visivyotumia maji wala kuunganishwa na mabomba ya maji taka Hatua Ambayo imeonekana kupunguza msambao wa magonjwa kama vile kipindupindu.

  • Ukosefu wa Ufahamu wa haki za afya ya uzazi ni kikwazo kikubwa ukanda wa Afrika

    17/09/2024 Duración: 10min

    Raia wengi bado hawawezi kufurahia haki zao za afya ya uzazi kutokana na ukosefu wa ufahamu Haki hizo ni pamoja na haki ya kuwa mzazi au la,kupata habari kuhusu afya ya uzazi ,kupata huduma bora za uzazi ,kushiriki mapenzi kwa njia stahiki na kuhudumiwa katika vituo vya afya kwa heshima

  • Matatizo ya kupata uja uzito miongoni mwa wanafamilia yanazidi kuongezeka

    03/09/2024 Duración: 10min

    Ripoti nyingi  zinaonesha wanawake pamoja na wanaume wanakabiliwa na changamoto za uzazi Wanandoa nyingi wanalazimika kukaa miaka mingi kabla kupata watoto ,kitu ambacho bado kinazingatiwa na jamii za Afrika kuwa ukamilifu katika kila ndoa au familia.Daktari bingwa wa uzazi dkt Dennis Miskella anaeleza  juhudi za kutafuta mtoto zinastahili kuwa ushirikiano kati ya mke na mumeweBaadhi ya sababu zinazohusishwa na hali hii ni kushiriki tendo la ndoa visivyo ,athari za baadhi ya mbinu za kupanga uzazi ,uvutaji sigara na pia unene wa kupitiliza

  • Wanawake wawafuga samaki kukwepa msambao hatari wa Ukimwi ziwa Victoria

    28/08/2024 Duración: 09min

    Mashirika ya kiraia yanayofanya kazi maeneo ya Kisumu nchini Kenya wanawasaidia wanawake kuachana na mpango wa kuuza miili yao ili kupata samaki Tabia hiyo inayofahamika kama ngono samaki kwa wakazi imekuwa ikichangia msambao wa virusi vya HIV

  • WHO imetoa mwongozo wa kupambana na MPOX katika mataifa ya Afrika

    20/08/2024 Duración: 10min

    Mikakati ambayo WHO inahimiza nchi za Afrika kukumbatia ni ubadilishanaji wa taarifa kuhusu ugonjwa wa Mpox ,ubainishaji sahihi na kampeni za chanjo Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ,kuna hofu ya msambao hatari wa MPox  unaohuishwa na vitendo vya ngonoWatalaam wa afya nchini DRC pia wanahimiza uhamasisho zaidi kuhusu ugonjwa huo ambao umesababisha vifo zaidi ya 500

  • MPOX yatangazwa janga la dharura la kiafya baada ya kasi ya maambukizi kuzidi

    20/08/2024 Duración: 09min

    Shirika la afya duniani ,WHO na taasisi ya kudhibiti magonjwa ya umoja wa Afrika ,CDC zililazimika kuchukua uamuzi mzito wa kutangangaza MPOX dharura ya kiafya Mataifa 16 ya Afrika kati ya 55 yameripoti visa vya MPOX mwaka huu ,CDC ikisema maambukizo yamepanda hadi asilimia 160 mwaka huu ukilinganishwa na mwaka 2023Virusi vya MPOX vimeripotiwa kujibadilisha  na kwa sasa msambao hatari wa virusi sugu zaidi unahusishwa na ngono

  • Bidhaa mpya za tumbaku zinauzwa kwa mwoneko bora, ladha ya kuvutia kuficha madhara yake

    06/08/2024 Duración: 09min

     Kuuza bidhaa za tumbaku za kisasa ,kama bidhaa zisizo na madhara ,kutumia ladhaa tamu na kutumia mitandao ya kijamii kuuza bidhaa hizi ni mbinu ambao kampuni za kutengeneza tumbaku zinatumia kuwavutia vijana na kuwa wateja wao wa kudumu. Kampuni hizi zinafadhili pia utafiti ambao unakinzani na utafiti wa taasisi za afya kuhusu madhara ya Tumbaku.Isitoshe kampuni hizi zinazalisha bidhaa ambazo mtumiaji anaweza kutumia zaidi ya moja .

  • Mbinu fiche zinazotumia sekta ya kuzalisha tumbaku kuendelea kudumu soko

    01/08/2024 Duración: 10min

    Kumeshuhudia juhudi makhsusi kutoka sekta ya Tumbaku zinazopinga sheria zinazodhibiti Tumbuka kama vile kupitia ushuri au sheria zenye adhabu kali Sekta hii pia imeonekana kurubuni serikali tofauti kwa kutoa msaada bila wao kufahamu lengo la sekta hiyo. Aidha kuna tafiti za kisayansi zinazofadhiliwa na sekta hii kukabili sayansi zinazorodhesha tumbaku na bidhaa za sigara kuwa zenye madhara makubwa ya kiafya

  • Simulizi kuhusu ugonjwa wa Endometriosis unaowasababishia wanawake maumivu

    24/07/2024 Duración: 10min

    Ugonjwa wa Endometriosis hudhihirika msichana anapovunja ungo na huja na maumivu makali kabla ,wakati na hata baada ya hedhi Lilian Leley ameishi na maumivu hayo kwa zaidi ya miaka thelathini.Amefanya upasuaji mara mbili na anatazamiwa kwenda kwenye operesheni nyingine hivi karibuni katika kujaribu kutafuta tiba ya ugonjwa wa EndometriosisAnasimulia masaibu yake ,ambapo anasema ndani ya mwezi huenda ni mzimu tu kwa siku 10

  • Fahamu kuhusu ugonjwa wa Endometriosis na changamoto za afya zinazofungamana nao

    16/07/2024 Duración: 10min

    Endometriosis hutokea wakati tishu kwenye ukuta  wa tumbo la  uzazi zinapopatikana katika maeneo mengine ya mwili ikiwemo mapafu ,utumbo na hata ubongo Endemotriosis huwa na dalili zinazofanana magonjwa mengine ya uzazi  na unaweza kubainika kupitia kipimo cha Laparoscopy ambapo tishu hizo zinachunguzwa moja kwa moja

  • Maandishi yenye tahadhari yatasaidia mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukizwa

    10/07/2024 Duración: 10min

    Bidhaa za vyakula au vinywaji zikiwa na machapisho ya kuonesha kuwa vina sukari nyingi ,chumvi nyingi  au mafuta mengi mnunuzi anakuwa na fursa ya kuchagua vema Watalaam wamesema lishe ni kiungo muhimu katika kupambana na magonjwa yasiyoambukizwa ambayo yanazidi kuongezeka na kuwa mzigo kubwa kwa jamii na mifumo ya afya

  • Mashujaa wa kupambana na Vitiligo wana matumaini makubwa ya jamii kuwaelewa

    10/07/2024 Duración: 09min

    Jamii nyingi bado hazielewi kuwa ugonjwa wa Vitiligo hauwezi kuambukizwa kwa kutangamana ,kugusana au hata kushiriki mlo

  • Dunia yaadhimisha siku ya ugonjwa wa ngozi - Vitiligo

    29/06/2024 Duración: 10min

    Vitiligo ni hali ya ngozi ambapo madoa meupe au mabaka yanaonekana. Inaweza kuathiri mtu yeyote, ikiwa ni pamoja na watoto na vijana. Sio hatari, si kama saratani ya ngozi au maambukizi unayoweeza kupata na kwa hiyo huwezi kuipata kutoka kwa mtu mwingine. Watu wengi wenye vitiligo wana afya nzuri. Baada ya muda, mabaka zaidi yanaweza kuonekana kwenye sehemu tofauti za mwili, hata kwenye nywele au ndani ya kinywa na pua. Mara nyingi huanza katika maeneo yaliyopigwa na jua. Takriban 1% ya dunia ina vitiligo

  • Muguka inaweza kusababisha madhara ya afya mtu anapokuwa mraibu

    21/06/2024 Duración: 10min

    Kumekuwa na mvutano kati ya serikali ,uongozi wa kaunti za Pwani ya Kenya ,kuhusu Muguka kupigwa marufuku kwa sababu za kiafya Wakulima ,wafanyabiashara  na wenyeji wa Embu wanaozalisha Muguka kwa kiasi kikubwa hata hivyo wanasema hawajapata madhara yoyoteHata hivyo watalaam wa afya wanaonya uraibu wa Muguka unaweza kudhuru afya

  • Sera kuhusu idadi ya watu inavyoathiri uchumi ,afya na hali ya maisha

    11/06/2024 Duración: 09min

    Mataifa ya Afrika bado yanaendelea kushuhudia kasi ya ongezeko la watu ijapokuwa chumi za Afrika hazifanyi vizuri inavyotakikana Watalaam wanaonya iwapo idadi ya watu haitodhibitiwa ,kupangiwa huenda mataifa mengi yakalemewa na idadi ya watu wanaowategemea wengineAidha kuna hatari ya sera za serikali kushindwa kukidhi mahitaji ya raia wake ,idadi inapokuwa kubwa

  • Juhudi za kuukabili ugonjwa wa Mycetoma kutumia dawa zilizofanyiwa utafiti Sudan

    08/06/2024 Duración: 10min

    Mycetoma ni mojawapo ya magonjwa yaliyopuuzwa ingawa unaendelea kuwaathiri wengi haswa watu wanaokaa maeneo kavu na jamii zilizotengwa Mycetoma hujidhihirisha kama donda ambalo haliponi bali linaendelea kukua na kuchimba sehemu athirika katika mwili

  • Mataifa ya Afrika yashinikiza mwongozo wa kukabiliana na hali ya dharura

    29/05/2024 Duración: 09min

    Mataifa wanachama wa shirika la afya duniani ,WHO yanayokongamano katika kongamano la afya ya 77 jijini Geneva yanataka kuwepo mwongozo wa afya kukabiliana na hali ya dharura baada ya janga la COVID 19  Mataifa haya yanasisitiza kuwepo usawa kwenye kuzalisha na matumizi ya sampuli za kutengeneza sampuli zinazochangiwa na nchi mbali mbaliAidha usawa kwenye ufadhili ,usambazaji wa chanjo mpya na chanjo zinazotumika wakati wa majanga Kongamano hilo pia linatazamiwa kuja na mwafaka kuhusu marekebisho kwenye sheria za afya za mwaka 2005

  • Matatizo ya afya ya akili yasipotatuliwa huwaathiri mustakabali wa watoto

    22/05/2024 Duración: 10min

    Watoto na  vijana walioshuhudia dhulma , kupata kiwewe,mara nyingi wanajikuta hawaamini katika uhusiano ,huwa waathiriwa wa dhulma za kimapenzi

  • Changamoto za afya ya akili miongoni mwa watoto na vijana Afrika

    14/05/2024 Duración: 10min

    Kumekuwa na ongezeko la idadi ya watoto na vijana wanaokabiliwa na changamoto za  afya  ya akili Kila mwezi Mei dunia huungana kufanya kampeni ya watu kuwa makini na afya zao za akili ili kuzuia changamoto zaidi za akili ambazo wakati mwingi huishia kwenye umauti na matatizo zaidi ya kiafyaWatalaam wa afya wanasema watoto na vijana pia nao hupatwa na changamoto hizi zinazohusishwa na afya ya akili ,matatizo hayo yakiwemo kiwewe na msongo wa mawazo.Daktari bingwa wa afya ya akili katika hospitali ya rufaa ya Kenyatta kitengo cha watoto ,Dkt Josephine Omondi anasema mazingira yanayochochea hali hii ni mizozo ya kifamilia ,matumizi mabaya ya mitandao ,shinikizo kutoka mazingira ya shule na pia matatizo ya kiafya yanayohusishwa na miaka ya awali ya mtotoMshauri Nasaha Naomi Ngugi anasema ni wakati wazazi wakakumbatia ukweli kuwa watoto na vijana huhitaji washauri nasaha na matibabu mengine ya matatizo ya afya ya akili

  • Mimba za utotoni zaendelea kuongezeka ukanda wa Afrika Mashariki

    08/05/2024 Duración: 10min

    Idadi kubwa ya wasichana wanaopata mimbo za utotoni wapo katika nchi za Afrika kwa mujibu wa shirika la afya duniani pia UNFPA Sababu zinazochangia mimba za utotoni ni pamoja na umaskini ,dhulma za kimapenzi ,ngono biashara na tamaduni hasi

página 1 de 2