Habari Za Un

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 8:30:11
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Episodios

  • Kenya tumepiga hatua kuhakikisha maendeleo ya ustawi wa jamii: Mary Wambui Munene

    14/02/2025 Duración: 04min

    Kikao cha 63 cha Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC kuhusu maendeleo ya ujamii kinakunja jamvi hii leo jijini New York Marekani baada ya majadiliano ya juma zima kuhusu maendeleo ya ustawi wa jamii, hatua zinazochukuliwa nan chi katika kufanikisha hilo na kuchagiza mshikamano wa kimataifa kutimiza lengo. Nchi mbalimbali zimetuma wakilishi kuanzia katika ngazi ya serikali, taasisi, mashirika yasiyo ya kiserikali na asasi za kiraia. Flora Nducha wa Idhaa hii amepata fursa kuzungumza na Mary Wambui Munene, mmoja wa washiriki kutokana Kenya. Ungana nao katika Makala hii

  • Mashambulizi yakishamiri DRC, sinfohamu yakumba wakimbizi

    14/02/2025 Duración: 02min

    Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, lina wasiwasi mkubwa kuhusu janga la kibinadamu linalozidi kuwa baya tena kwa kasi kubwa huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kwani kushindwa kufikia wahitaji kumekwamisha ufikishaji misaada ya harakati inahoyitajika. Anold Kayanda na ripoti kamili.

  • 14 FEBRUARI 2025

    14/02/2025 Duración: 11min

    Hii leo jaridani tunaangazia machafuko na hali ya wakimbizi wa ndani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Makala inaturejesha hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na mashinani inatupeleka nchini  Jamhuri ya Africa ya Kati (CAR), kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, lina wasiwasi mkubwa kuhusu janga la kibinadamu linalozidi kuwa baya tena kwa kasi kubwa huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kwani kushindwa kufikia wahitaji kumekwamisha ufikishaji misaada ya haraka inahoyitajika..Katika kitongoji cha Komanda jimboni Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, doria za pamoja zinazoendeshwa na walinda amani wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO na jeshi la serikali FARDC zimeimarisha usalama kwenye maeneo ya raia.Makala leo inaturejesha hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kwenye mkutano wa 63 wa Baraza la Kiuchumi na Kijamii ECOSOC kuhusu maendeleo ya jamii. Flora Nducha amepata fursa ya kuzung

  • Doria za pamoja za MONUSCO na FARDC huko Ituri DRC zaimarisha usalama

    14/02/2025 Duración: 01min

    Katika kitongoji cha Komanda jimboni Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, doria za pamoja zinazoendeshwa na walinda amani wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO na jeshi la serikali FARDC zimeimarisha usalama kwenye maeneo ya raia. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

  • Jifunze Kiswahili: maana za neno “MSUMBI”

    13/02/2025 Duración: 57s

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo fursa ni yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa      nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana za neno “MSUMBI”

  • 13 FEBRUARI 2025

    13/02/2025 Duración: 11min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kumulika siku ya redio duniani, maudhui yakiwa Radio na Tabianchi, na ni kwa vipi chombo kinachodaiwa kutwamishwa na maendeleo ya teknolojia kinaendelea kusaidia kuelimisha umma kuhusu madhara ya mabadiliko ya tabianchi, Teonas Aswile wa TBC Taifa nchini Tanzania anaeleza.Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambapo hali inazidi kuwa tete na leo Mkurugenzi Mtendaji wa shirkika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, Catherine Russell, ameelezea wasiwasi mkubwa kuhusu kuongezeka kwa ghasia mashariki mwa mwa  nchi hiyo katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini, ambapo watoto na familia wanakabiliwa na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.Naibu mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masiala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA nchini Sudan Edmore Tondhlana akizungumza na UN News amesema hali nchini Sudan inaendelea kuwa janga la kibinadamu wakati vita ikishika kasi na watu wakiendelea kufurushwa makwao. Amesema "

  • Akibomoa kibanda chake Goma DRC, mkimbizi asema ana hofu kurejea Saké

    12/02/2025 Duración: 01min

    Baada ya waasi wa M23 jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupatia wakimbizi waliokuwa wamesaka hifadhi kambini mjini Goma, wawe wamerejea makwao ndani ya saa 72 kuanzia juzi jumatatu, mamia wameanza kutii amri hiyo.Miongoni mwao ni Kibira Bakulu, baba wa watoto 5, aliyekimbia mapigano eneo la Saké, mwezi Februari mwaka jana, takriban kilomita 10 kutoka Goma.Akiwa katika harakati za kubomoa kibanda chake katika kambi ya nane ya CEPAC Mugunga huko Goma, Bwana Bakulu anasema walishangaa, bila kuwa tayari, kuambiwa warudi walikotoka."Tumepatiwa saa 72 tuwe tumeondoka na kurejea Saké, kwani vita vimeisha. Sisi hatua uhakika kamili kwa sababu tuliondoka Saké kutokana na vita. Kama inabidi kusukumwa tuondoke, hatuna la kuchagua,” amesema Bwana Bakulu.Ana hofu ya kurejea Saké, akisema, “kule tulikuwa tunaishi Sake na tukirejea tutaishi vipi? Tunaomba viongozi wajitahidi watusaidie ili watuhakikishia usalama.Alipoeleza hali halisi amesema, “ hii siku ya leo hapa unaniona, watu w

  • Redio imetusaidia kufikisha elimu kwa umma kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi

    12/02/2025 Duración: 03min

    Ikiwa kesho Februari 13 ni Siku ya Kimataifa ya Redio, makala inatupeleka jijini Nairobi, Kenya ambako ambako Kevin Keitany wa redio washirika wetu Domus FM kwa kuzingatia kuwa kesho Februari 13 ni Siku ya Kimataifa ya Redio, ametutumia maoni ya vijana wawili wanaozungumzia namna redio imewasaidia kusambaza ujumbe wao kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

  • Wakimbizi Goma waanza kufungasha virago huku wakiwa na hofu

    12/02/2025 Duración: 01min

    Baada ya waasi wa M23 jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupatia wakimbizi waliokuwa wamesaka hifadhi kambini mjini Goma, wawe wamerejea makwao ndani ya saa 72 kuanzia juzi jumatatu, mamia wameanza kutii amri hiyo licha ya hofu inayowakabili ya kule wanakotakiwa kurejea. Miongoni mwao ni Kibira Bakulu, baba wa watoto 5, aliyekimbia mapigano eneo la Saké, mwezi Februari mwaka jana, takriban kilomita 10 kutoka Goma.

  • 12 FEBRUARI 2025

    12/02/2025 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia matokeo ya maandamani nchini Bangladesh, na machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Makala inatupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi na ofisi ya haki za binadamu (OHCHR) imefichua kuwa viongozi wa juu wa serikali ya Bangladesh walihusika moja kwa moja katika ukandamizaji wa maandamano makubwa yaliyoitikisa nchi hiyo mwaka 2024 na kusababisha vifo vingi.Baada ya waasi wa M23 jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupatia wakimbizi waliokuwa wamesaka hifadhi kambini mjini Goma, wawe wamerejea makwao ndani ya saa 72 kuanzia juzi jumatatu, mamia wameanza kutii amri hiyo licha ya hofu inayowakabili ya kule wanakotakiwa kurejea.Makala inatupeleka jijini Nairobi, Kenya ambako ambako Kevin Keitany wa redio washirika wetu Domus FM kwa kuzingatia kuwa kesho Februari 13 ni Siku ya Kimataifa ya Redio, ametutumia maoni ya vijana wawili wanaozungumzia namna r

  • Ripoti yabainisha ushiriki wa viongozi wa juu katika ukandamizaji Bangladesh

    12/02/2025 Duración: 01min

    Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi na ofisi ya haki za binadamu (OHCHR) imefichua kuwa viongozi wa juu wa serikali ya Bangladesh walihusika moja kwa moja katika ukandamizaji wa maandamano makubwa yaliyoitikisa nchi hiyo mwaka 2024  na kusababisha vifo vingi. Flora Nducha na taarifa zaidi

  • 11 FEBRUARI 2025

    11/02/2025 Duración: 10min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Uganda kumulika ni kwa nini Uganda imekivalia njuga Kiswahili akieleza mwandishi wetu wa Uganda John Kibego ambaye amezungumza na mwandaaji mwenza wa kongamano hilo Dkt. Kisembo Ronex Tendo, Mkurugenzi wa shirika la Afrika Mashariki Fest.Umoja wa Mataifa na wadau wanasalia na wasiwasi mkubwa kufuatia amri iliyotolewa Jumatatu na waasi wa M23 huko jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ya kupatia wakimbizi wa ndani saa 72 wameondoka kwenye kambi mjini Goma na viunga vyake, na kurejea vijijini mwao.Katika Ukanda wa Gaza ambako Rolando Gomez, Mkuu wa Mawasiliano kwenye Ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva Uswisi, amezungumza na waandishi wa habari akimnukuu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akisema lazima kuepusha gharama zozote zinazoweza kuibuka iwapo uhasama utaanza upya Gaza kwani italeta janga kubwa.Na akihutubia viongozi huko Paris Ufaransa kwenye mkutano wa Kuchukua Hatua kwa Akili Mnemba ili inufa

  • Wapalestina wahitaji ufadhili na mshikamano wa kimataifa - Tom Fletcher

    10/02/2025 Duración: 03min

    Huko Mashariki ya Kati Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Dharura, OCHA Tom Fletcher alifanya ziara ya siku tatu huko Ukingo wa Magharibi na Gaza ili kujionea hali halisi ya raia. Katika Sharon Jebichii amefuatilia ziara yake na kutuandalia makala hii..

  • Kakuma - Je, unafahamu kwamba nyenje ni chanzo cha protini?

    10/02/2025 Duración: 01min

    Katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma, kutokana na ufadhili wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), kundi la vijana wanajishughulisha na ufugaji wa wadudu nyenje (Crickets) ili kukabiliana na changamoto ya utapiamlo miongoni mwa watoto wachanga. Anold Kayanda na maelezo zaidi.

  • 10 FEBRUARI 2025

    10/02/2025 Duración: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia hali ya wahamiaji na wakimbizi nchini Libya, na wakimbizi wajasiriamali katika makazi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya. Makala inatupeleka Jerusalemu Mashariki, na mashinani nchini Chad, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM, limeeleza mshtuko mkubwa na wasiwasi wake kufuatia kugunduliwa kwa makaburi mawili nchini Libya walimozikwa wahamiaji kadhaa, baadhi yao wakiwa na majeraha ya risasi.Katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma, kutokana na ufadhili wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), kundi la vijana wanajishughulisha na ufugaji wa wadudu nyenje (Crickets) ili kukabiliana na changamoto ya utapiamlo miongoni mwa watoto wachanga.Katika makala Sharon Jebichii anakupeleka Mashariki ya Kati kumulika ziara aliyofanya Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Dharura, OCHA huko Ukingo wa Magharibi na Gaza ili kujionea hali halisi ya raia.Na mashinani kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu, UNFPA, nampisha

  • IOM: Miili ya wahamiaji 39 yakutwa kwenye makaburi mawili Libya

    10/02/2025 Duración: 02min

    Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM, limeeleza mshtuko mkubwa na wasiwasi wake kufuatia kugunduliwa kwa makaburi mawili nchini Libya walimozikwa wahamiaji kadhaa, baadhi yao wakiwa na majeraha ya risasi. Flora Nducha na taarifa zaidi

  • Mabaya zaidi nchini DRC yanakuja iwapo hatutauchukua hatua, aonya Mkuu wa Haki za Binadamu wa UN

    07/02/2025 Duración: 02min

    Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, leo akizungumza katika Kikao Maalum cha Baraza la Haki za Binadamu kinachofanyika jijini Geneva, Uswisi, ameonya kuwa ghasia zinazoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zinaweza kuwa mbaya zaidi ikiwa hazitashughulikiwa. Flora Nducha na taarifa zaidi.

  • Juhudi za mahakama Tanzania kutekeleza Lengo namba 16 ya SDG

    07/02/2025 Duración: 03min

    Leo katika makala Hamad Rashid wa Redio washirika KidsTime FM ya mkoani Morogoro Tanzania aanaangazia kuhusu namna Tanzania inaendelea kufanikisha Lengo Namba 16 la Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa linatilia mkazo upatikanaji wa amani, haki na taasisi imara kwa kupunguza mrundikano wa mashauri au kesi mahakamani, kuwezesha upatikanaji wa haki kwa makundi maalumu katika jamii.

  • 07 FEBRUARI 2025

    07/02/2025 Duración: 10min

    Hii leo jaridani tunaangazia hali ya haki za binadamu nchini Jamhuri ya kidemokasia ya Congo DRC, Na masuala ya afya nchini Jamhuri ya Congo, au Congo-Brazaville. Makala inatupeleka nchini Tanzania, na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, leo akizungumza katika Kikao Maalum cha Baraza la Haki za Binadamu kinachofanyika jijini Geneva, Uswisi, ameonya kuwa ghasia zinazoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zinaweza kuwa mbaya zaidi ikiwa hazitashughulikiwa.Wananchi wa Jamhuri ya Congo, au Congo-Brazaville, ni mashuhuda wa jinsi shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO limewasaidia kukabiliana na ugonjwa wa macho na ngozi unaosababishwa na nzi mweusi wanaozaliana kwenye mito na vijito, ugonjwa ambao uliathiri shughuli zao za kijamii na kiuchumi kutokana na muwasho wa kila mara na upofu.Katika makala Hamad Rashid wa Redio washirika KidsTime FM ya mkoani Morogoro Tanzania anaangazia kuhusu namna Tanzania in

  • Congo-Brazaville yaelekea kutokomeza ugonjwa wa ngozi na macho

    07/02/2025 Duración: 01min

    Wananchi wa Jamhuri ya Congo, au Congo-Brazaville, ni mashuhuda wa jinsi shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO limewasaidia kukabiliana na ugonjwa wa macho na ngozi unaosababishwa na nzi mweusi wanaozaliana kwenye mito na vijito, ugonjwa ambao uliathiri shughuli zao za kijamii na kiuchumi kutokana na muwasho wa kila mara na upofu. Assumpta Massoi na taarifa kamili.

página 1 de 5